Tangaza na Abd Da Hustler

Champagne aahidi mageuzi makubwa FIFA


Jerome Champagne
Mgombea wa kiti cha urais wa shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, Jerome Champagne, amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa kutoa kadi ya chungwa wakati wa mechi za soka, ili kuruhusu marefa wa mechi kuwaruhusu wachezaji waliofanya madhambi kuondolewa uwanjani kwa muda.
Champagne mwenye umri wa miaka hamsini na tano kutoka Ufaransa, aliyasema hayo siku ya Jumatatu wakati alipoanzisha kampeini yake ya kumrithi Sepp Blatter kama rais wa FIFA.

Uchaguzi wa urais wa FIFA utafanyika mjini Zurich Juni mwaka wa 2015.Amesema ikiwa atashinda atapendekeza vilabu vya soka kuadhibiwa ikiwa wachezaji wake watahoji maamuzi ya refa na vile vile kuchunguza uwezekano wa kutumia teknolojia kutatua maamuzi muhimu.
Miongoni mwa mapendekezo mengine aliyoyasema ni kuthibiti idadi ya wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa na vilabu, kutangazwa kwa mshahara wa rais wa FIFA na maafisa wengine wakuu.
Aidha ameahidi kuwa atafutilia mbali sheria ya sasa inayotoa adhabu tatu kwa mchezaji ambaye atafanya madhambi katika eneo la hatari.
Kuambatana na sheria ya sasa mchezaji yeyote anayefanya kosa katika eneo la hatari, hupewa kadi nyekundi moja kwa moja na pia kupigwa marufuku ya kutocheza mechi mbili zinazofuata.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment