Tangaza na Abd Da Hustler

Wahudumu wa afya wauawa Pakistan


Taliban wamekuwa wakiwaua wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya Polio Pakistan
Watu waliojihami katika mji wa Karachi nchini Pakistan, wamewaua kwa kuwapiga risasi wahudumu watatu wa afya wakiwemo wanawake wawili waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio.
Hili ni shambulizi la hivi karibuni likiwalenga wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya Polio au ugonjwa wa kupooza.

Mwanamke mmoja alifariki papo hapo wakati mwingine alifariki akipelekwa hospitalini.Walioshuhudia shambulio hilo walisema waliona watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wakiwa wanaendesha Pikipiki wakiwapiga risasi wahudumu wa afya waliokuwa wanatoa Chanjo hiyo kwa watoto wadogo.
Shambulizi hilo ni pigo kubwa kwa juhudi za Pakistan kupambana na ugonjwa huo unaolemaza.
Kando na Afghanistan na Nigeria, Pakistan ni moja ya nchi ambako ugonjwa wa Polio ni janga kubwa.
Wapiganaji wa Taliban wanapinga chanjo ya ugonjwa wa kupooza na wamekiri kuwaua wafanyakazi wa afya wanaotoa chanjo hiyo nchini Pakistan.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment