Mabondia Francis Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Mohamed Matumla
'Snake JR' wamesaini mkataba wa kupambana April 26 katika ukumbi wa PTA,
Sabasaba jijini Dar es salaam.
Akizungumzia mpambano huo promota wa mchezo wa masumbwi, Ally Mwazoa amesema ameingia nao mkataba mabondia hao kwa kuwa anajua wanaweza mchezo wa masumbwi na ni mafundi wa mchezo huo.
“Najua kuna watu wengi walitamani kudhamini mchezo huo lakini bahati imeniangukia mie” Alisema Ally Mwazoa.
Mpambano huo utakaopigwa April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi ambapo mwana dada Lulu Kayage atamvaana na Halima Ramadhani siku hiyo kwa ajili ya kuhamasisha wanawake wenzao wajitokeze katika mchezo wa masumbwi.
Baada ya kusaini mkataba huo bondia Miyeyusho alitamba kuendeleza ubabe katika familia hiyo ambapo alisema atamchakaza kama alivyo mchakaza baba yake mdogo Mbwana Matumla ambaye amecheza nae mara tatu na kupigwa mara mbili ambapo mpambano wa mwisho ulikuwa na shamu shamu nyingi kila upande Miyeyeyusho alibuka mshindi kwa point.
Nae Nohamed Matumla, alijibu mapigo kwa kusema Miyeyusho anamuheshimu kwa kuwa yeye ni mkubwa kiumri, hata hivyo atampa kichapo kikali kama alivyompatia mdogo wake Doi Miyeyusho ambaye mara ya kwaza alipigwa kwa K,O raundi ya pili katika pambano lililofanyika DDC Keko na mara ya pili pia K,O ya raundi ya pili katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
“Siwezi kushusha rekodi yangu kwa kupigwa na Miyeyusho akitaka kujua mimi ni mkali zaidi yao amulize pia Nassibu Ramadhani ambaye nilimpatia kipigo kibaya sana na kunifanya ninyakue pikipiki.” Alisema Mohamed Matumla.

0 MAONI :
Post a Comment