Tangaza na Abd Da Hustler

Audio: Mtoto wa marehemu George Tyson 'Sonia' atoa ujumbe mzito wa majonzi kumuaga baba yake

Jana simanzi ma majonzi vilitawala katika viwanja vya Leaders Club wakati mamia ya watu walipokuwa wakiaga mwili wa muongozaji wa filamu na vipindi vya televisheni, George Tyson aliyefariki katika ajali ya gari.
Moja kati ya matukio yaliyowatoa machozi mamia ya watu waliohudhuria katika tukio la kumuaga Tyson, ni pale mtoto wake wa kike aitwae Sonia alipokuwa akitoa neno/ujumbe wa kumuaga baba yake.
Sonia aliongea kwa majonzi maneno yaliyosababisha watu wengi watokwe machozi.
“You were kind na rafiki yangu kipenzi. Ulikuwa mtu ambaye ni rahisi kuongea nae na kunielewa. Daima ulikuwa unanitunza na kunidekeza. Na mara ya mwisho kuonana na wewe wiki iliyopita ulinambia ni jinsi gani nimekufanya uwe pride na mimi. And moreover I sing…I take a breath away. Na ninakuahidi, sitaacha kuimba kwa ajili yako. Nataka ufahamu kwamba nitakupenda milele. I will always Love You dad. Rest In Peace.”
Sonia ni mtoto wa marehemu aliyempata na muigizaji Monalisa ambaye pia ni mtangazaji wa 100.5 Times Fm.
Misikilize hapa:
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment