Majogoo wa jiji Liverpool wamefanikiwa kumsajili mchezaji wa
pili ndani ya juma hili baada ya kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji
kutoka nchini Uingereza Rickie Lambert, aliyekuwa anamilikiwa na klabu
ya Southampton.
Liverpool ambao waliukosa ubingwa wa nchini Uingereza msimu wa mwaka 2013-14 kwa kuzidiwa kete na matajiri wa mjini Manchester, Man city wamefanikiwa kumsajili kiungo kutoka nchini Ujerumani Emre Can, akitokea Bayer Leverkusen.
The Reds wamekamilisha usajili wa mchezaji huyo ambae ni sehemu ya timu ya taifa ya Ujerumani chini ya umri wa miaka 21, kwa ada ya uhamisho wa paund million 4.4.
Mtendaji mkuu wa klabu ya Bayer Leverkusen, Michael Schade, saa kadhaa zilizopita alithibitisha taarifa za kuuzwa kwa Emre Can, katika mtandao wa klabu hiyo.
“Sasa ninathgibitisha dhahir taarifa za kuuzwa kwa kiungo Emre Can, baada ya kukamilisha biashara na uongozi wa klabu ya Liverpool ambao tangu jumatatu usiku tulikuwa kwenye mazungumzo nao.” Taarifa ya Michael Schade kupitia mtandao wa klabu imeonekana hivyo.
Emre Can, anaondoka BayArena, huku akiacha kumbu kumbu ya kucheza michezo 29 na kufunga mabao matatu mara baada ya kusajiliwa na uongozi wa klabu ya Bayer Leverkusen mwaka 2012 akitokea FC Bayern Munich.

0 MAONI :
Post a Comment