Tangaza na Abd Da Hustler

Ronaldinho Gaucho kucheza soka Afrika

Katika hali ya kushangaza raisi wa klabu ya Zamalek ya nchini Misri  Mortada Mansour, ametangaza kufanya mazungumzo ya kumsajili aliyewahi kuwa mchezaji bora wa dunia Ronaldo de Assis Moreira *Ronaldinho Gaucho* ambae kwa sasa anaitumikia klabu ya Atlético Mineiro ya nchini kwao Brazil. Raisi wa Zamalek alitangaza mpango huo wakati akihojiwa kwenye kituo cha televisheni cha taifa cha nchini Misri, ambapo amesema anaamini watafanikiwa kukamilisha mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo.
Hata hivyo mtangazaji Khaled Ghandour aliyekuwa anamuhoji Mortada Mansour, alionyesha kushangazwa na taarifa hizo na kujikuta akiuliza mara mbili mbili, lakini jibu aliloambulia kutoka kwa kingozi huyo lilikuwa la kushangaza pia.
 Mortada Mansour alirejesha swali kwa mtangazaji huyo kwa kumuuliza kwa nini anashangazwa na taarifa hizo, ama anataka kuona wanamsajili Barack Obama?
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment