Tangaza na Abd Da Hustler

Update: Moto mkubwa wateketeza soko la Karume Dar, Jerry Slaa na mwenyekiti wa soko wazungumza

Soko la mitumba la Karume la Dar es Salaam limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo (June 11 Usiku).
Mwenyekiti wa soko hilo, Jumanne Song’o ameeleza kuwa asilimia 85 ya soko hilo ndiyo iliyoteketea kabisa na kwamba ni wafanyabiashara 3,000 waliokuwa wakifanya shughuli zao kisheria lakini kwa sasa idadi yao ni zaidi ya 10,000.
Ameeleza kuwa moto huo umesababisha hasara kubwa na athari kubwa kwa wafanyabiashara hao kwa kuwa wengi wao hutumia fedha za mikopo kuendesha biashara.
Nae Meya wa Ilala, Jerry Slaa aliyefika katika eneo la tukio amewataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu na kwamba halmashauri itashirikiana nao kwa hali na mali kufahamu chanzo cha moto huo.
Mheshimiwa Slaa amesisitiza kuwa wafanyabiashara hao wapo katika soko hilo kisheria na kwamba atahakikisha wanaendelea kuwepo.
Akieleza kuhusu athari za mikopo walizopata wafanyabiashara hao, Mheshimiwa Slaa amesema watafanya kikao cha dharua leo mchana kitakachowajumuisha viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Ilala ili tathimini ya thamani ya mali iliyoteketea pamoja kujadili mengine muhimu ya kuwasaidia wafanyabiashara hao wanaoishi kwa kutegemea mikopo.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment