Victoria iliicharaza AFC Leopards ya Kenya mabao 2-1
Timu ya Chuo Kikuu Cha Victoria
kutoka Uganda imeibuka mshindi wa mashindano ya kandanda ya kombe la
Cecafa Nile Basin yaliyomalizika Jumatano wiki hiimjini Khartoum, Sudan.
Victoria imeshangaza wengi kwa kutwaa kombe hilo baada ya kushinda AFC Leopards ya Kenya mabao 2-1 mjini Khartoum,Sudan.Ilikua ni shangwe na hoi hoi kwa wachezaji wa Victoria kwani ni mwaka jana tu timu hiyo iliundwa ikilinganishwa na Leopards ambayo ilianzishwa mwaka wa 1964..
Victoria ilifuzu kushiriki mashindano hayo ya Sudan kwa kuibuka mshindi wa Uganda Cup, na katika ligi kuu ya Uganda ilimaliza ya pili..
Al Shandy ya Sudan ilimaliza ya tatu kwa kuicharaza Academie Tchite ya Burundi mabao 4-1 kwenye mechi ya kuamua mshindi wa tatu..
0 MAONI :
Post a Comment