Tangaza na Abd Da Hustler

Mambo matatu makubwa Rage aliyoiachia Simba – kikiwemo kiasi hiki cha pesa benki

RageALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, ameshusha pumzi na anakwenda kupumzika huku akidai kuiacha Simba na mambo matatu ya kihistoria.

Kwanza ni  akaunti ya klabu yenye kitita cha Sh420 milioni, pili  ni Uwanja wa Bunju na tatu makubaliano yake na Benki  ya Posta kuhusiana na kadi za wanachama ambazo kama uongozi mpya utakuwa makini, klabu itaingiza pesa nyingi kupitia mtindo huo.
Akikokotoa kiasi hicho cha Sh420 milioni, Rage alisema kati ya hizo zimo Sh60 milioni za mauzo ya Shomari Kapombe aliyesajiliwa na Azam FC, Sh160 milioni za kodi ya mapango ya jengo la Simba lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na Sh100 milioni za wadhamini.
Akizungumza na Mwanaspoti pia Rage alionyesha hisia zake juu ya kero alizokuwa anakutana nazo alipokuwa madarakani, alisema:  “Kuongoza klabu kubwa kama Simba ni lazima ujitoe, hata hivyo vurugu kubwa za klabu ambazo zinatokea huwa zinasababishwa na njaa tu. Hivyo kumaliza muda wangu nashukuru maana nakwenda kupumzika.”
Source: Mwanaspoti
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment