Tangaza na Abd Da Hustler

Ndoa ya Arsenal FC na kampuni ya Puma yathibitishwa rasmi

Uongozi wa klabu ya Arsenal umetangaza rasmi kuanza mkataba wa kutumia vifaa vya michezo vya kampuni ya Puma baada ya mkataba wa miaka kumi na kampuni ya Nike kufikia kikomo hapo jana.
Arsenal ambao ni mabingwa wa kombe la FA mwaka 2014, wamethibitisha kuanza kutumia vifaa vya kampuni ya Puma kutokana na mkataba na kampuni hiyo kuanza kutumia rasmi hii leo July mosi.
Kampuni ya Puma itakuwa ikihusika kuivisha timu ya Arsenal jezi zenye nembo ya kampuni hiyo na pia itasaidia katika mambo mengi ambayo yamekubaliwa kimkataba.
Arsenal imethibitisha taarifa za kuanza kutumia vifaa vya kampuni ya Puma kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment