Jana Desemba 10 Watanzania walimpokea kwa shangwe kubwa aliyekuwa mshiriki wa BBAHotshots Afrika Kusini, Idris.
Ushindi wa Idris ilikuwa habari njema, Miss World je?
Mshiriki wetu kwenye Mashindano ya Miss World, Happiness Watimanywa saa chache zilizopita ameweka ujumbe huu Instagram; “Tanzania Asanteni kwa support na uzalendo. Tuendelee mpaka namba Moja!!!!! #vote #PigaKura #DownloadTheApp #MissWorld2014”– @happinesswatimanywa
Katika list hiyo, Happiness ameshika nafasi ya tisa katika kumi bora ya top ten Miss World People’s Choice.
Hakika Desemba hii itakuwa mwezi wa sherehe kubwa kwa Tanzania iwapo tukimfanikisha Happiness kurudi na ushindi huu nyumbani.
TANZANIA, Happiness Watimanya - Contestant Profil…: http://youtu.be/OAANobXSsqA
0 MAONI :
Post a Comment