Tangaza na Abd Da Hustler

Miss World 2014 ndio ilikuwa leo, matokeo yote yapo hapa pamoja na picha

Miss World 2014, Rolene Strauss aliyeiwakilisha South Africa akifurahi baada ya kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014.

Leo December 14 kwenye Historia ya mwaka 2014, Mashindano makubwa yaMiss World 2014 yalikuwa yakifanyika London, Uingereza ambapo washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Tanzania, Happiness Watimanywaakiwa mmoja ya washiriki hao.

Mpaka leo asubuhi matokeo ya kura ambazo zilikuwa zikipigwa na watu zilimuweka mwakilishi huyo kuwa katika nafasi ya pili, akitanguliwa na Miss Thailand ambapo iwapo Happinessangekuwa namba moja basi ilikuwa moja kwa moja aingie kwenye Top 10 ya mashindano hayo.

Kutokana na Hapiness kupitwa kura naMiss Thailand hakufanikiwa kuingia kwenye Top 10, huku katika wale waliotajwa ni wawakilishi wawili pekee, mmoja wa South Africa na mwakilishi wa Kenya waliofanikiwa kuingia Top 10.

Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss amefanikiwa kuvuka hatua zote na hatimaye kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014, nafasi ya pili ikishikwa na Miss Hungary, Edina Kulcsar na nafasi ya tatu kushikwa na Miss USA, Elizabeth Safrit.

Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment