Obama Atoa Somo La ubaguzi Wa Rangi Kwa Wamarekani
Rais Barack Obama wa Marekani amewasihi vijana nchini humo kuwa thabiti katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi lakini pia kuwa wavumilivu kwani mageuzi hayapatikani kwa urahisi.
Kauli yake inajiri wakati maandamano yakiendelea kwenye miji ya Washington, New York na Berkeley dhidi ya uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama kutowashtaki maafisa wa polisi wazungu waliohusishwa na vifo vya wanaume wenye asili ya Kiafrika-wamarekani weusi hivi karibuni Eric Garner na Michael Brown
Rais Obama amesema maandamano ni muhimu kuikumbusha jamii kwamba maguezi bado hayajafanyika Lakini ameongeza kwamba maandamano hayo hayana maana iwapo yatakumbwana ghasia.
Zaidi ya watu 200 wamekuwa wakiandamana katika miji mbali mbali hasa mjini New York wakilalamika kwamba polisi wanawalenga wamarekani weusi baada ya visa kadhaa vya vijana wamarekani weusi kuuawa katika siku za hivi karibuni.
0 MAONI :
Post a Comment