Sep Blatter
Shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa wiki ijayo watapiga kura ili kuamua kuwekwa hadharani kwa ripoti ya uchunguzi wa mgogoro wa rushwa katika utoaji zabuni za kuandaa michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 na 2022. Mkutano huu utakao fanyika jijini Marrakesh nchi morocco utatoa maamuzi ya kuweza kusambazwa ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya rushwa katika kutoa nafasi ya wenyeji wa michuano ya kombe la dunia. Viongozi wa soka chini ya mapendekezo ya kamati ya maadili ya Fifa ilisisitiza sio rahisi kutolewa kwa ripoti hiyo kwa sababu za kisheria. Fifa wamewapa nafasi Urusi kuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 na Qatar kwa mwaka 2022,Uteuzi wa nchi hizi unaonekana umegubikwa na mazingira ya rushwa.
0 MAONI :
Post a Comment