Wiki iliyopita tulisikia stori kwamba Rais Robert Mugabe alimtuhumu Makamu wake Joyce Mujuru kwamba alikuwa akipanga mikakati ya kumuua.
Jana Desemba 09 kafanya maamuzi ya kulipangua Baraza la Mawaziri na pia kafanya maamuzi ya kumsimamisha kazi Joyce Mujuru japo Makamu huyo wa Rais japo muda mfupi uliopita alikanusha yale madai kwamba alikuwa na mango wa kumuua Rais huyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa Mugabe pia amewafukuza Mawaziri wanane na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Misheck Sibanda ambaye amesema amemfukuza kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wake.
Joyce Mujuru, Makamu wa Rais aliyesimamishwa kazi na Rais Mugabe na aliyewahi kushutumiwa kwamba alipanga njama za kumuua.
Maamuzi yake kwa Mujuru imesemekana ni kutokana na kuwepo taarifa kwamba alikuwa akiandaliwa na chama kama mrithi wa Rais huyo.
Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90 yuko madarakani tangu Zimbabwe ipate uhuru mwaka 1980 na yupo katika.
0 MAONI :
Post a Comment