![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWYH2n1uP689cNa-aruIGrgk0q2EXX0rxQhB2CQUrt8LyezgiA7iW5MB_y1uMedDfuhCSxJG7DTBR7U8Kh_jEEa29_w1YAvPoE9c2bbilUgSuSN3qBFmN1ezISA6QHzIDuHyQQVjnL-cUc/s400/omar.jpg)
MWIGIZAJI wa filamu nchini, omary Clayton, ameibuka kidedea katika kipengele cha msanii bora wa kiume kwenye tuzo za Califonia Online Viewers Choice Awards (COVCA) zilizotolewa usiku wa kuamkia jana huko Marekani.
Nyota huyo ni moja ya waigizaji wakuu waliofanya vizuri kwenye filamu inayoitwa Dogo Masai iliyomfanya Omary Clayton kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Tuzo hiyo ilikuwa inawaniwa na wakali kama vile Veron Aldershoff wa Marekani, Dario Merlini wa Ufaransa, Seppe Cosyns wa Ubelgiji na Eric Calderon wa Costa Rica.
0 MAONI :
Post a Comment