![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUFzMYym1Xw2MitMN8ROuwARJzTaB1BeUkiv5YPUDXhtQN2NvqN_L-DJmRYmUXeKU4vAKqsctN2ye5Ibs6cmrxFitrSbKZLlxnB_U7zJ5DDPRtXbWFLxMqZDLODEzv7Ce39_FQO36fdgdT/s400/diamondnayamotoband-559x520.jpg)
Wakati Yamoto Bendi wakiendelea kutoa burudani mji wa Washington DC,imefanikiwa kuwania tuzo za Kora 2016,ikiwa kwenye kipengele cha’Most Promising Male Artist of Africa’.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella alisema kwanza anamshukuru Mungu kwa vijana kufanya onesho la pili juzi Washington DC,pia kufanikiwa kuingia katika tuzo za Kora.
Fella ambaye ni diwani wa Kata ya Kilungule alisema ni kitu kikubwa kwa bendi yake kuingia tuzo za kimataifa na kinazidi kuipandisha bendi yake ambayo sasa ipo Marekani kwa ziara ya maonesho maalum.
Kwa upande wa ziara ya bendi yake nchini Marekani alisema vijana hao watafanya onesho la mwisho Desemba 12,katika mji wa Houston na baadaye kurejea nchini kwa kazi zao nyingine.
0 MAONI :
Post a Comment