Tangaza na Abd Da Hustler

Majambazi yarusha Risasi ovyo Bunda, yaua mchoma ‘vitumbua’.


Wakazi wa mji wa Bunda mkoani Mara hivi sasa wanaishi maisha ya hofu baada ya kundi la majambazi kuvamia na kumuua muuza vitumbua.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 1:40 usiku na kusababisha taharuki kwa wananchi  ambao walilazimika kukimbia   kunusuru uhai wao.
Majambazi hayo yalivamia katika eneo    jirani na Benki ya NMB Tawi la Bunda na kufyatua risasi ambayo ilimuua kijana huyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, majambazi hayo pia  yalivamia katika vibanda vya M-pesa vilivyoko katika eneo la kituo cha  zamani cha mabasi mjini Bunda   yakiwa yanarusha risasi ovyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi, alisema   iliwalazimu askari waliokuwa zamu katika benki ya NMB kujibu mapigo kwa kufyatua risasi.
“Risasi nyingi ni za polisi waliokuwa lindoni pale benki ya NMB waliona wajibu mapigo kwa kufyatua risasi,” alisema Kalangi.
Mmoja wa wafanyabiashara ambao kibanda chake cha M-pesa kilivamiwa na majambazi hayo, Omar Rashid, alisema   watu hao waliokuwa na bunduki walimteka na kumtaka atoe fedha  zote alizokuwanazo.
Alisema  majambazi hayo yalichukua zaidi ya Sh 800,000 zilizokuwa kwenye droo na simu yake ya mkononi ya kutolea huduma ya M-Pesa  iliyokuwa na zaidi ya Sh milioni moja.
“Ilikuwa kama saa moja na dakika 45 hivi nilishutukia wanapiga risasi, nikiwa bado ninashangaa wakavamia katika kibanda changu wakitaka niwape fedha zote nilizokuwa nazo.
“Kabla sijatoa tu mmoja alikuwa na kama nyundo akataka kunipiga nikatoa droo ya fedha nikawapa na wakachukua na simu yangu ya M-Pesa,” alisema Rashid.
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment