Jana ilikuwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa, ya Actress daraja
la kwanza kwenye kiwanda cha filamu Bongo aitwae Jacqueline Wolper.
Katika kusheherekea siku yake hiyo muhimu, Wolper kama mkazi wa Kimara Golani jijini Dar es salaam akaamua kudhamini uchimbaji wa Kisima kusaidia kupunguza kero ya maji katika eneo hilo.
“Kuanzia mwaka juzi nimekua na desturi ya kushirikiana na watu siku yangu muhimu ya kuzaliwa Mwaka juzi nilipata nafasi ya kukaa na watoto yatima na mwaka jana kituo cha wazee Mwaka huu nimeamua kugusa maisha ya watu wengi zaidi Kwahivyo kwa kutafakari jinsi gani tatizo la maji ni kubwa, nimeamua kutumia kidogo nilichonacho kujenga kisima chenye uwezo wa kuhudumia watu 3500 katika shule ya msingi eneo la Golani Kimara. Wananchi wa huku wamekua wakipata shida ya maji sana na wenye uwezo wamekua wakinunua ndoo moja kwa tsh 1000, ambayo ni bei kubwa kugharamikia maji. Hili ni tatizo kwakweli, sio hapa tu bali maeneo mengi nchi nzima. Nimeona niwashirikishe jambo hili wapendwa wangu wote kwakua tuna nafasi ya kusaidia hata kama kidogo ila naamini “even a penny can change the world” Ukitoa kidogo na mwingine pia akatoa basi lazima kutakua na mabadiliko Tunaweza kuanza kufanya na kubariki maisha ya wanaotuzunguka kidogo kidogo Tuanze leo. Maji ni haki ya kila binadamu. Lets save lives,help bring water.” ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Mkali huyo ameshukuru ushirikiano alioupata kutoka kwa Diwani wa kata hiyo na Mbunge wa Ubungo Saeed Kubenea, pamoja na baadhi ya wakazi wa Golani Kimara.

0 MAONI :
Post a Comment