Bunge la Ugiriki limepiga kura kuunga mkono mswada wa
sheria, unaohusu maandalizi ya kuzifuta nafasi 25,000 za
ajira katika sekta ya umma. Sheria hiyo ni mojawapo ya
masharti yaliyowekwa na wakopeshaji wa kimataifa, yaani
Umoja wa Ulaya na Shirika la fedha ulimwenguni, IMF.
Mswada huo ulipata wingi wa kura zilizohitajika
kuuidhinisha, ambazo ni angalau 151 katika bunge lenye
viti 300. Kura hiyo bungeni imepigwa muda mchache tu
kabla ya ziara ya waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang
Schäuble. Watu wanaopinga hatua hiyo walifanya
maandamano kuupinga mswada huo. Waandamanaji
walidai wanapigania haki ya tawala za mitaa na ile ya
kuwapa watu nafasi ya kujiamulia mambo yao wenyewe.
About Unknown
Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
0 MAONI :
Post a Comment