Umoja wa Mataifa umesema unatazama upya msaada
wake kwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
baada ya ripoti kuwa jeshi hilo linawatesa mateka wa kundi
la M23 lililowakamata, na kuzitendea maovu maiti za wale
waliouawa. Jeshi la serikali ya Kongo lilitumia helikopta
kuwashambulia waasi hao kwa siku tatu mfululizo, na
maelfu ya wakaazi wamevihama vijiji vyao kuepuka
mapigano. Makabiliano mapya baina ya jeshi la serikali na
waasi wa M23 yaliibuka Jumapili iliyopita.
Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon,
imesema amehangaishwa na taarifa hizo. Aidha, katika
taarifa hiyo, Ban aliitaka serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kuwafikisha mbele ya sheria
wanajeshi waliohusika na uhalifu huo. Umoja wa Mataifa
ulirejesha ushirikiano na jeshi hilo, baada ya kufikishwa
mahakamani kwa maafisa wawili waliotuhumiwa kuwabaka
wanawake katika eneo la Minova, mwezi Februari mwaka
huu.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 MAONI :
Post a Comment