Tangaza na Abd Da Hustler

Rais wa Somalia anusurika kuuawa

      Raisi wa Somalia    Hassan Sheikh Mohamud 
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amenusurika jaribio la kumuuwa lililofanywa na wanamgambo wa al-Shabab wenye mafungamano na al-Qaida. Radio ya taifa ya Somalia na pia duru za kidiplomasia zimeeleza kuwa msafara wa rais huyo umewasili salama katika bandari ya Merka, baada ya shambulio hilo la kuvizia.
Al-Shabab ambayo ilikuwa ya kwanza kutangaza kutokea kwa shambulio hilo, imesema imeweza kuharibu magari kadhaa yaliyokuwa katika msafara huo.
Msemaji wa kundi hilo  Abdulaziz Abu Musab ameliambia shirika la habari la AFP kuwa shambulio hilo la kuvizia limetokea karibu na kijiji cha Buffow,  karibu na bandari ya Merka, katika eneo ambalo lilikuwa ngome ya al-Shabab, umbali wa km 100 kusini mwa mji mkuu Mogadishu.      
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment