Tangaza na Abd Da Hustler

Zimetajwa Kuwa Ni Beef Nane Za Kitoto Za Hiphop.


Beef ni jambo ambalo lipo kwenye muziki wa hiphop na hutumika kwa manufaa tofauti kama promotion, umaarufu na kupata heshima mtaani. Rappa kama 50 Cent ametajwa kuwa ni msanii bora zaidi kwenye kutumia beef kujinufaisha.

Hizi Beef ambazo zimetajwa kuwa za kitoto kwenye hiphop.

Beef ya rapper Tyga na Drake iliyotokana na Tyga kusema hampendi Drake kwamba sio mtu REAL.

  Floyd Mayweather alisema  50 Cent hana seheu tena kwenye muziki wa rap na hana album inayofanya vizuri sokoni.Baadae 50 Cent alianzisha kampuni ya kusimamia mapambano ya ngumi.

Ndio beef ya rap yenye umaarufu zaidi kwa sasa, Drake na Chris brown hawaelewani baada ya kumpigania Rihanna mwaka 2012 na sasa Drake amelaumiwa tena na Chris Brown kwa kumchukua mpenzi wake K Tran.

Meek Mil alilalamika kuwa pamoja na kuwa kwenye lebel moja na Wale, jamaa hajamsaidia kutangaza album yake kwenye twitter wale kwenye interview zake, Meek anaamini Wale anamchukia.

Drake na Common wote wanampenda mwanamke moja ‘ Serena Williams’ mcheza tennis maarufu duniani.

Manager wa Justin Bieber ‘Scooter’ alimwambia msanii wake asifuatane na rapper wa Young Money ‘Lil Twist’ sababu hana nidhamu na atamfundisha tabia mbaya.

Wakati Jay Z yuko mapumziko mshkaji wa rappa  Cam’ron ‘Jim Jones’ alitangaza kuwa makamu wa rais waRoc-A-Fella records atakuwa Cam’ron na ameteuliwa na  Dame Dash ambaye kwa wakati huo alikuwa mmiliki wa lebel hio akishirikiana na Jay Z. Miezi michache baadae Dash aliuza hisa zake na Jay Z akawa mmiliki bila kumpa cheo chochote Cam’ron.

Meek Mill na Cassidy walipishana baada ya Meek kusema anaweza kushinda Freestyle na Cassidy. Haikwenda mbali baada ya Meek kuambiwa kuwa hawezi kushinda na atapoteza heshima kama atashindwa na Cassidy

Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment