Karegeya alikuwa mshirika wa karibu sana wa Rais Paul Kagame kabla ya kutofautiana
Chama cha upinzani cha Rwanda
National Congress leo kinatarajiwa kuandaa maandamano ya raia wa Rwanda
wanaoishi Afrika Kusini hadi makao ya ubalozi wa taifa hilo mjini
Pretoria kulalamikia mauaji ya aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi Kanali
Patrick Karegeya .
Karegeya alipatakina akiwa amefariki dunia katika hoteli moja mjini Johanesburg mwezi Disemba mwaka uliopita.Ubalozi wa Rwanda nchini Afrika Kusini umesema kuwa hautatishika na maandamano hayo.
Karegeya alikuwa mkuu wa zamani wa ujasusi nchini Rwanda, na alipatikana amenyongwa katika hoteli moja mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mjane wa Karegeya amesema kuwa atazikwa nchini humo.
Taulo iliyokuwa na damu ilipatikana katika chumba ambapo maiti ya Karegeya ilipatikana na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi. Hata hivyo hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa.
Muaji ya Karegeya, yamesababisha madai dhidi ya serikali ya Rais Kagame kusema kuwa huenda ilihusika na mauaji hayo.
Karegeya alikuwa mshirika wa karibu sana wa Kagame kabla ya kutofautiana naye.
0 MAONI :
Post a Comment