Tangaza na Abd Da Hustler

Diamond kushuhudia Live show ya Pharrell Williams, Drake, Lil Wayne, Usher kwenye tuzo za BET 2014

Mwaka huu ni tofauti kidogo na miaka ya nyuma kwa Tanzania kwa kuwa ukitaja BET Awards 2014 ni lazima utupie jina la Diamond kizalendo kwa kuwa ni moja kati ya wanaoweza kupanda kwenye jukwaa hilo.
Waandaaji wa tuzo hizo wametaja majina ya wasanii watakaotumbuiza kwenye jukwaa la tuzo hizo, June 29 ambapo majina Pharrell Williams, Drake, Lil Wayne, na Usher Raymond yamethibitishwa kuwa katika orodha hiyo.
Wasanii wengine watakaopiga show live kwenye jukwaa la BET Awards ni Trey Songz na Jennifer Hudson.
 Diamond Platinumz ni mmoja kati ya wasanii waliotajwa kuwania tuzo hizo na kwa jinsi ambavyo maoni ya awali ya mitandao ya kijamii ya BET inaonesha mkali huyo wa Ngololo Style anaongoza.
Endapo Diamond atapata tuzo hiyo atakuwa amepanda jukwaa ambalo wamepanda wasanii hao wakubwa na huenda ikawa ni ishara nzuri kwake…mwakani tunaweza kumuona akipiga show kwenye jukwaa hilo. Huwezi Jua!
Share on Google Plus

About Unknown

Naitwa Abdalla Ngowi, Napenda Michezo na kukupa habari mbalimbali kutoka katika kila kona ya ulimwengu huu!, karibu ABD da Hustler
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 MAONI :

Post a Comment