Diego Costa ambae ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, amesema wazazi wake wameliafikia suala la yeye kuitumikia timu ya taifa ya Hispania na wanafurahishwa na hatua hiyo kutokana na kufahamu kwamba soka ndio maisha yake ya kila siku.
Amesema ana mahusiano mazuri na wazazi wake na hata siku moja hawakuwahi kumkalipia kutokana na maamuzi aliyochukua, hivyo hata yeye anajihisi furaha kuwa miogoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alichukua maamuzi ya kuitumikia timu ya taifa ya Hispania mwaka huu, baada ya kukasirishwa na mpango wa kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari wa kumuacha katika kikosi cha nchi hiyo kilichoshiriki michuano ya kombe la mabara ya mwaka 2013.
Kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque alimuita kwenye kikosi chake Diego Costa, February 28 mwaka huu kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Italia.
0 MAONI :
Post a Comment