Watu hao waliingia kama raia wema wanaohitaji msaada wa polisi lakini ghafla walimvamia askari huyo na kumkata mapanga kasha kumpora bunduki aina ya SMG ikiwa na risasi 30.
Watu hao walipora pia risasi za akiba 41.
Baada ya kujeruhiwa vibaya na watu hao marehemu Ngonyani alikutwa akiwa katika hali mbaya na kukimbizwa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ambapo alifariki wakati akipata matibabu.
Wengine waliojeruhiwa katika tukio hilo ni mgambo Mariam aliyejeruhiwa shingoni na kichwani, na mwingine aliyetajwa kwa jina la Venance aliyejurihiwa mgogoni kwa risasi.
Msikilize mwandishi wa Times Fm, Masau Bwire akiripoti kuusu tukio hilo na utamsikia pia Kamanda wa polisi wa Pwani.
0 MAONI :
Post a Comment