Picha za hivi karibuni za Vera Sidika kwenye mitandao ya kijamii
Swala la kubadili rangi ya ngozi
limekuwa kama msumari moto, kunao wanaoliunga mkono na wale
wanaolipinga swala hilo katu hawawezi kulifanya.
Baadhi wanasema kuwa ni wanawake wasiojithamini na kujiamini pekee ndio wenye kujichubua ngozi.Mmoja wa wasichana hao ni Vera Sidika anayejulikana sana nchini Kenya na Afrika mashariki kwa kuwa na makalio makubwa ambayo ndiyo yaliyompa umaarufu wake baada ya kuonekana katika wimbo mmoja wa video uitwao 'You Guy' ambao baadaye ulipigwa marufuku nchini Kenya.
Picha za awali kabla ya Vera kujichubua ngozi
Vera anajulikana kwa kuwa na mazoea ya kujipiga picha hasa za makalio yake na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. Vara analinganishwa sana na Kim Kardhashian hasa kwa sababu ya umbo lake.
Kazi ya Vera hasa ni ya uwanamitido lakini mbali na hilo Vera hulipwa ili kufika kwenye karamu mbali mbali , kwenye disco na katika hafla mbali mbali za watu mashuhuri. Yeye pia hulipwa kuwa katika kanda za video za wanamuziki maarufu Afrika Mashariki.
Alifichua kupitia televisheni Ijumaa kuwa alitumia maelfu ya dola kubadili rangi ya ngozi yake na kujifanya mweupe.
Shughuli hiyo aliifanyia nchini Uingereza na ilimgharimu karibu milioni 15 pesa za Kenya, hizo ni dola 170,000 na kwamba tayari kuna watu wengi wanaotaka sana kujichubua ngozi na kufanana na Vera, kwa mujibu wa mwanadada huyo.
Vera ni mwanamitindo na anapanga kufungua duka la kuuzwa bidhaa za urembo
Mtindo wa wanawake kujichubua ni swala tata nchini Kenya. Sio kama India ambako vipodozi vya kujichubua huuzwa wazi wazi. Nchini Kenya bidhaa hizo, huuzwa kimagendo.
Wataalamu wanasema, wanawake wengi wanaendelea kujichubua licha ya hatari za bidhaa zinazouzwa kimagendo.
Swala la wanawake kijichubua barani Afrika lilianza kujadiliwa waziwazi pale ambapo msanii raia wa Cameroon Dencia kuzindua rasmi bidhaa zake za kuchubua ngozi ziitwazo, Whitenicious.
0 MAONI :
Post a Comment