Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jennifer Lopez amewasili
nchini Brazil tayari kwa shamrashamra za ufunguzi wa fainali za kombe la
dunia ambazo zitachukua nafasi kwenye uwanja wa Sao Paolo.
J-Lo amewasili nchini humo baada ya kubadili maamuzi ya kutishiriki katika shamrta shamra hizo ambao aliutoa siku tatu zilizopita, lakini jana mchana alithibitisha ushiriki wake.
Sababu kubwa ya mwanamuziki huyo kubadili msimamo wake, imetokana na ukaribu uliopo dhidi mashabiki wake ambao walihitaji kumuona jukwaani akishirikiana na wasanii wengine kwa ajili ya kuimba wimbo maalum wa fainali za mwaka huu uliopewa jina la "We Are One (Ole Ola)"
Wasanii walioshirikiana na J-lo kutengeneza wimbo huo ni Pitbull, pamoja na mwenyeji Claudia Leitte.
Wasanii 6000 wa fani mbali mbali za sanaa wanatarajiwa kushiriki katika shamra shamra za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia ambazo pia zitahudhuriwa na maafisa wa soka dunia kote wakiongozwa na raisi wao Sepp Blatter.
Baada ya shamra shamra hizo mchezo wa ufunguzi ndipo utachezwa kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia kutoka barani Ulaya.
Muamuzi kutoka nchini Japan Yuichi Nishimura amepewa jukumu la kupuliza kipyenga katika mchezo huo.
Kwa mara ya mwisho timu hizo kukutana katika michuano ya kombe la dunia ilikua mwaka 2006 kule nchini Ujerumani na matokeo yalikuwa mazuri kwa Brazil ambao waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo Ricardo Izecson dos Santos Leite kaka.
Michezo ya kesho
Arena das Dunas, Natal
13 June 2014
Mexico Match 2 Cameroon
Muamuzi: Wilmar Roldán (Colombia)
Arena Fonte Nova, Salvador
13 June 2014
Spain Match 3 Netherlands
Muamuzi: Nicola Rizzoli (Italy)
Arena Pantanal, Cuiabá
13 June 2014
Chile Match 4 Australia
Muamuzi: Noumandiez Doué (Ivory Coast)

0 MAONI :
Post a Comment